The House of Favourite Newspapers

Tshishimbi: Simba Njooni Mezani

Pappy Tshishimbi.

KIUNGO kipenzi cha mashabiki wa Yanga, Pappy Tshishimbi jana asubuhi alirejea kwao DR Congo kwa mapumziko ya wiki mbili lakini akasema kwamba kama Simba wakija mezani rasmi atawafikiria.

 

Akizungumza na Mhariri Mtendaji wa GPL, Saleh Ally (pichani kushoto) walipokutana kwenye Uwanja wa Ndege wa Nairobi, Kenya jana Jumamosi, Tshishimbi alisema; “Simba hawajanifuata rasmi, nasikia tu. Lakini kama wako siriazi nitawasikiliza kwa kuwa soka ni biashara na ndiyo kazi yangu.”

 

“Mchezaji profeshno inapofika kwenye suala kama hilo kuna wakala wako analishughulikia, lakini niko tayari kama tutafikia makubaliano sahihi,” alisisitiza Tshishimbi ambaye ana mkataba na Yanga.

 

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera naye amekwenda zake Ufaransa kuweka mambo sawa huku akisubiri ripoti yake ifanyiwe kazi na uongozi.

Comments are closed.