TTCL YAZINDUA ENEO MAALUM LA MAPOKEZI MAKAO MAKUU

Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa kwanza kulia) akizungumza na wageni mara baada ya kuzinduwa eneo la mapokezi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wageni waalikwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria uzinduzi wa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

…Waziri Kindamba (kulia) akimuonesha Mhandisi Omari Rashid Nundu eneo maalumu la historia ya mawasiliano lililopo eneo la mapokezi mpya ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa leo. 

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akimmiminia shampeni kuashiria uzinduzi wa eneo la mapokezi lililozinduliwa leo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa mapokezi hiyo ya kisasa. 

Sehemu ya wahudumu katika eneo la mapokezi hiyo wakionesha baadhi ya simu za zamani zilizotumiwa kipindi cha nyuma. 

Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (mwenye koti). 

 

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezindua eneo la mapokezi ya shirika hilo lililopo Makao Makuu ya Shirika, jijini Dar es Salaam. Eneo hilo lililoboreshwa kwa ukarabati wa kisasa limeongezewa sehemu maalum ya maonesho na historia ya mawasiliano nchini ikiwa ni kutoa elimu zaidi kwa jamii.

 

 

Akizindua eneo hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya  TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kwenda sambamba na maboresho makubwa yanayofanywa ndani ya shirika la TTCL.

 

Alisema muonekano mpya wa eneo la mapokezi katika Jengo la Makao Makuu ya Shirika hilo ni kielelezo muhimu cha jinsi gani TTCL mpya inavyo wathamini wateja wake kwa kuwapa kipaombele.

 

” Tunatambua kuwa bila wao, huduma na bidhaa zetu hazitakuwa na maana yoyote wala hatutaweza kutimiza wajibu wetu kwa Umma na Taifa letu.  Hii ndiyo sababu ya msingi inayotufanya siku zote tuwape wateja wetu nafasi ya kwanza katika kila mipango tunayoipanga na kuitekeleza,” alisema Mhandisi Nundu.

 

Aliwataka menejimenti na wafanyakazi wote wa TTCL, kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Shirika na hasa kipengele cha Huduma kwa Wateja ili kukidhi matarajio na mahitaji ya Wateja wake.

 

Aidha aliongeza kwa mwaka 2019, TTCL Corporation imejipanga vyema kuhakikisha kuwa huduma za shirika hilo inasambaa zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo Wananchi wote watazimudu.

 

“Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa.”

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba awali akizungumza, alisema; “Tunafanya maboresho makubwa katika majengo ya Ofisi za watumishi, Majengo ya kuhifadhia Mitambo na Teknolojia pamoja na Maduka na Vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja Nchi nzima.”

 

“Hadi kufikia sasa, Majengo ya TTCL katika Mikoa kumi tayari yamefanyiwa ukarabati mkubwa huku Maduka na Vituo vya huduma kwa Wateja 15,” aliongeza kiongozi huyo.

 

Pamoja na hayo Bw. Kindamba alisema kukamilika kwa ukarabati katika eneo hilo la mapokezi lililofanyiwa maboresho kunaongeza uwezo wa kuwahudumia Wateja sambamba na kukabiliana na ushindani kutoka kwa Watoa huduma wengine.

Toa comment