Tuhuma za ukwepaji kodi… 40 watiwa mbaroni Dar

IMG_7727Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD, ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.

IMG_7643Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

IMG_7694Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015.

IMG_7612Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es Salaam.

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.

Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.

Pia kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu.

Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika.

hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,

Amewasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Loading...

Toa comment