Vidonda vya mdomoni ni miongoni mwa matatizo yanayowasumbua watu wengi. Badala ya kuhangaika kutumia dawa za hospitali, unaweza kutumia tiba za asili na tatizo likaisha.
Mahitaji
-Tui la nazi
-Maji ya uvuguvugu
-Aloevera
-Chumvi
-Nyanya
Kuna nazi kisha kamua tui la nazi. Litumie kusukutua mdomoni mara tatu hadi nne kwa siku mpaka vidonda viishe.
Unaweza pia kutumia maji ya uvuguvugu na ya baridi kwa wakati mmoja, yaani unasukutua kwa maji ya uvuguvugu kwa sekunde 30, unayatema na kusukutua kwa maji ya baridi kwa dakika tatu, endelea kubadilisha hivyohivyo mara tatu hadi nne. Rudia zoezi mara tatu kwa siku.
Chukua ute wa aloevera, uchanganye kwenye maji ya uvuguvugu kisha sukutua mdomoni mara tatu kwa siku.
Kula nyanya mbivu ambazo hazijapikwa angalau tatu kwa siku, unaweza pia kutengeneza juisi ya nyanya na kuitumia kusukutua mdomoni, mara tatu hadi nne kwa siKu.
Njia iliyozoeleka na wengi ni kuchanganya chumvi kwenye maji ya uvuguvugu kisha sukutua kwa sekunde thelathini hadi dakika moja, rudia mara tatu kwa kila tukio na rudia mara tatu kwa siku nzima.
Comments are closed.