Tuishangilie Simba kwa faida ya nchi

JUMAMOSI timu ya Simba itakuwa uwanjani kuvaana na AS Vita kwenye mchezo mgumu wa kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kama Simba watashinda mechi hii basi ni asilimia 100 watakuwa wamefuzu kwa lakini pia ni heshima kubwa kwa Tanzania na ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa kuwa ndiyo timu pekee iliyobaki.

 

Kutokana na hali hiyo ni vyema sasa tukabadilika kidogo na kuziunga mkono timu zetu zinazoshiriki
hatua hiyo na hii itakuwa heshima ya pekee kwenye soka la nchi hii. Kufuzu kwa Simba ni faida pia kwa Yanga kwa kuwa timu hizo ndiyo kubwa ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara
michuano ya kimataifa.

 

Mashabiki wa Yanga Jumamosi wanatakiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya kuiunga mkono Simba ili kuliletea taifa sifa kubwa. Kwenda na kuishangilia Vita haliwezi kuwa jambo zuri kwa
kuwa wote ni Watanzania na tunatakiwa kuhakikisha tunaweka uzalendo mbele zaidi ya mambo mengine yote kama ambavyo yamekuwa yakifanya mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka.

Toa comment