visa

TUKIO LA KUTAKA KUTAPELIWA LAMPA FUNZO JOKATE

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa, tukio la mwanaume Omari Chuma kutaka kumtapeli lililomtokea hivi karibuni, limempa fundisho kubwa maishani.

Akizungumza na Amani, Jokate alisema kupitia tukio hilo amejifunza kutomuamini mtu yeyote hata kama atakuwa na maelezo ambayo yanaonesha kumjua sana. “Nimejifunza kwa kweli, sitamuamini mtu tena.

Nimeongeza umakini, nimejidhatiti pia katika suala la ulinzi,” alisema Jokate. Jamaa huyo alimuingia Jokate na kutaka kumtapeli hivi karibuni lakini hata hivyo alishtukiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zaidi za kisheria.
Toa comment