The House of Favourite Newspapers

TUKIO LA MO DEWJI KUTEKWA, WAZIRI MAKAMBA AHOJIWA NA POLISI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana usiku Oktoba 21, 2018 lilimhoji kwa saa kadhaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba,  kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (Mo).
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amethibitisha na kusema waziri huyo aliruhusiwa kuondoka baada ya kuhojiwa.

Awali taarifa zilisambaa mitandaoni kuwa waziri huyo amekamatwa na polisi kwa mahojiano, jambo ambalo Makamba amekanusha.

“Sijakamatwa na polisi. Niko salama,” ameandika Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Baadaye akafafanua…

Alichokiandika Makamba siku ya tukio la kutekwa kwa Mohammed Dewji.

Makamba ni miongoni mwa watu waliopata taarifa mapema za kupatikana kwa bilionea huyo na kuandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mo Dewji alitekwa Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi na kupatikana Oktoba 20 saa nane usiku, baada ya waliomteka kumtelekeza katika viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche

Comments are closed.