The House of Favourite Newspapers

Tume Kenya Yaonya Kuhusu Whatsapp, Wananchi Wapinga

0

 

MKUU wa Tume ya Mshikamano na Uadilifu nchini Kenya (NCIC), Francis Ole Kaparo, ametoa onyo kwamba watu wanayaotumia makundi ya mtandao wa WhatsApp wawe makini katika kusambaza habari wanazoandika hususan sasa kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini humo mwezi Agosti mwaka huu.

 

Tume hiyo imefichua kwamba kuna makundi 21 yanayosambaza habari za uchochezi na kwamba inayafuatilia nyendo zake.

 

Hata hivyo, wananchi wameishambulia tume hiyo wakisema imeshindwa kuwakabili wanasiasa na badala yake inawageukia wao. Wengi wao wamesema tume hiyo inafanya hivyo kwa vile imeshindwa kudhibiti masuala ya usalama katika mchakato huo kuelekea uchaguzi.

 

Wananchi wengi wanaona hiyo ni njia ya kuwafunga midomo, ambapo Kaparo naye amesema hilo likiendelea mitandao ya kijamii inawezwa kufungwa.

 

Hivi majuzi mtu mmoja alikamatwa mjini Eldoret nchini humo kwa kila kilichosemwa kueneza maneno ya chuki kwenye mtandao wa Facebook ambapo alipofikishwa mahakamani alikana na yuko nje kwa dhamana.

Swali lililopo kuhusu jambo hilo ni: NCIC inatimiza wajibu wake au inatafuta kisingizo?

 

Said Aliyetobolewa Macho na Scorpion, Mkewe Waanza Kugawana Mali, Varangati Laibuka

Leave A Reply