TUMEKWISHA! HIVI NDIVYO WENYE SIMU ZENYE PICHA ZA NGONO WATAKAVYONASWA

KAMA hujaisikia mbiu, ni vyema ukutangaziwa wazi kwamba wale am­bao bado tunahifadhi picha na video za ngono kwenye simu zetu za mkononi kinyume na amri ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ya kututaka tuzifute TUMEKWISHA; Uwazi lina full stori.  

 

Hakiyanani hakuna wa kupona kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya vyombo vya usalama na Mam­laka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’.

Wasiojua mbinu za kiusalama za kuzuia uhalifu kwenye simu wamekuwa wakibishabisha kwamba: “Simu yangu ninayo mwenyewe, nimeifunga kwa namba za siri; hao TCRA wa­nawezaje kujua kuma nina picha chafu na kunikamata?”

Kauli hii ni sawa na mbwa ana­vyoweza kujipeleka kwa chatu huku akipepesa mkia akidhani yu salama kumbe anakwenda kumezwa, Uwazi limeambiwa teknolojia ya kisasa inaweza kumbaini mtu aliyetuma au kuhi­fadhi picha alizotumiwa kirahisi kabisa na kumtia mbaroni.

Image result for PAU MAKONDA NA SIMU ZENYE PICHA ZA NGONO

MSIKIE MTAALAMU KUTOKA TCRA

“Kufanya kazi ya kuwafua­tilia wahifadhi picha za ngono kwa wingi wao inaweza kuwa ngumu, lakini haishindikani pale inapotakiwa wahusika kupa­tikana. “Watu wanatakiwa kujua, vitu vingi siku hizi vinahifadhiwa kwa mfumo kama vinasaba DNA kwamba kila kitu kina utambul­isho wake ambao hauingiliani na mwingine.

 

“Mfano kwenye simu kuna namba ya utambulisho inaitwa IMEI, hii kila simu inayo ya kwake, hazifanani, kwa msingi huo tukitaka kumjua mtu anaye­tumia simu aina fulani tunaweza kuanzia kwenye kuangalia hiyo namba na kufuatilia mambo mengine kwa kufuata sheria.

 

“Kwa hiyo hata hizi picha unazoziona nazo zina namba ya utambulisho ambao haufanani  na nyingine, wataalam wakiika­gua wanaweza kujua ilipigwa lini, kutumia kifaa gani, ilikuwa saa ngapi na eneo gani?

“Ukipata taarifa hizi nili­zokutajia ni rahisi kufuatilia nani mhusika na pengine kama kuna aliowatumia unamjua mmojammoja na kuwakamata inawezekana,” kilisema chanzo chetu kinachofanya kazi TCRA katika kitengo cha Tehama.

 

WATAKAMATWA WOTE?

Kwa mujibu wa chanzo hi­cho inaelezwa kuwa kufanya oparesheni ya kuzuia uhalifu si lazima watu wote wakamatwe lakini wakipatikana nguli wa mambo hayo na kushugulikiwa tatizo linaweza kumalizika. “Unajua pengine kutokana na wingi wa watu kuwa na picha za ina hiyo ndiyo maana wengi wanajifariji kuwa serikali haiwezi kuwakamata wote.

 

“Nilipita sehemu moja mitaa ya Kinondoni (jijini Dar) nikam­sikia kijana mmoja anawaambia wenzake agizo la mkuu wa mkoa ni la kutishia watu kwa sababu haiwezekani kuwamata wote wenye picha hizo kwani wanaweza kujaza mahabusu. “Lakini kama nilivyosema, lengo si wote kukamatwa, lakini wakipatikana mia au hamsini wakachukuliwa hatua si itakuwa fundisho kwa wen­gine!” Chanzo kilifafanua.

 

SHERIA INASEMAJE?

Sheria inakataza mtu kuhifa­dhi picha chafu kwa sababu anaweza kusababisha zikach­apishwa jambo litakalomtia hatiani kwa kufungwa miaka 10 au kulipa faini ya shilingi milioni thelathini.

Aidha ni kosa pia kumuone­sha sha picha au video za ngono mtu ambaye si mke au mpenzi wako, jambo linalowapa mamlaka polisi kumtia mbaroni mtu yeyote anayehifadhi picha chafu na kumfikisha mahaka­mani.

 

POLISI WANENA

Kufuatia agizo la mkuu mkoa wa Dar lililozua gumzo la kuwataka watu wote wenye picha chafu kuzifuta kabla ya Novemba 5 mwaka huu, jeshi la polisi kwa upande wake nalo liko tayari kuanza kazi ya kuwasaka watuhumiwa.

 

Akizungumza na Uwazi afisa wa polisi kutoka kitengo cha upelelezi kanda maalumu ya Dar ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema: “Kusaka wahalifu kuko kwa njia nyingi ikiwemo ya kushuku, sasa kama mtu anasema atakuwa na simu yake ameiweka password, polisi akimshuku si anamuita na kumwambia aifungue ili ikaguliwe.

 

“Ugumu uko wapi, ni wazi wengi watakamatwa, wataho­jiwa na wale watakaopatikana na kosa watapelekwa mahaka­mani. “Hata kama mimi si mse­maji wa jeshi la polisi nilikuwa nawaomba wananchi na hasa watumiaji wa simu za mkononi kutii sheria bila kushurutishwa, haya mapicha ya ngono ya nini kwenye simu? Si wayafute?”

 

Kaimu Meneja Mawasil­iano TCRA, Semu Mwakan­jala alipotafutwa kwa lengo la kutolea ufafanuzi wa namna mamlaka hiyo itakavyoweza kuwanasa watuhumiwa wa kuhifadhi picha chafu haku­weza kupatikana kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa. Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro alipotafut­wa hakupatikana kuzungumzia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar.

 

FARAGHA YA MAWASILIANO YATAJWA

Wakati mjadala wa kuwatia mbaroni watuhumiwa wa kuhi­fadhi picha chafu ukiendelea na hofu ya simu za watu kupekuliwa, baadhi ya watu wamekuwa na hofu kuwa huenda mambo haya yakaleta uvunjifu wa katiba ya nchi. Ibara ya 16 ya Katiba ya nchi kifungu 1 inasema; Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi

 

kwa naafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyum­ba wake, pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi. Hata hivyo katika kifungu kidogo cha pili cha ibara hiyo kinaweka mazingira ambayo faragha ya mtu inaweza kuingiliwa bila kuathiri kifungu cha kwanza.

 

“Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yanaweza kuin­giliwa bila ya kuathiri ibara hii.

 

MEZA YA MHARIRI

Kutokana na hali halisi ilivyo, meza ya mhariri inawashauri watumiaji wa simu za mkononi kuwa makini na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano na badala yake kutumia mawasiliano kama njia ya kuboresha maendeleo na siyo kutumiana picha za ngono.

Stori: RICHARD MANYOTA, Dar

Loading...

Toa comment