The House of Favourite Newspapers

Tumia Kitunguu Maji Kutibu Kucha Yenye Uvimbe

WATU wengi hupata tatizo la kuchomoa vikucha vya pembeni ambapo baada ya kufanya hivyo hupata tatizo la kuvimba na kutokewa na usaa, watu wengine utasikia kidole kina mdudu. Je, unajua tiba yake asili? Ungana nami nikujuze zaidi tiba yake.

KITUNGUU MAJI

Chukua kitunguu maji kikatekate vipande kisha weka kwenye kidole chenye tatizo kisha weka bandeji funga kidole hicho baadaye funga kisha acha usiku kucha. Kitunguu kinasaidia kuondoa maumivu yote ya kwenye kidole.

LIMAO

Limao nayo inasaidia kwa kiasi kikubwa, unachotakiwa kufanya ni kukatakata vipande vyemb-amba vya limao kisha weka kwenye kidonda alafu funga na bandeji lala nayo mpaka asubuhi.

HYDROGEN PEROXIDE

Hydrogen Peroxide ni maji yale ya kusukutua mdomoni ambayo unaweza kutumia kama tiba kwenye tatizo hilo, unachotakiwa kufanya ni kuosha eneo lililoathirika na sabuni yoyote ya maji kisha chukua pamba loweka kwenye dawa hiyo weka kwenye kidonda fanya hivyo kutwa mara tatu.

Comments are closed.