The House of Favourite Newspapers

Tumia Limao na Mzaituni kwa Kucha Bomba

0

lemon

Ni kitu kilicho wazi kwamba wanawake wengi hasa wa mjini wanapenda kufuga kucha. Katika hilo, baadhi wanatamani sana kucha zao ziwe safi na nyeupe lakini hawajui watumie njia gani.

Leo shosti wenu nimewaletea namna ya kuzifanya kucha zako ziwe na muonekano mzuri kwa kutumia limao na mafuta ya mzaituni.

Unafanyaje?
Chukua kijiko kimoja kikubwa cha juisi ya limao, changanya na mafuta ya mzaituni vijiko vitatu kwenye bakuli moja.
Weka kwenye ‘microwave’ kwa muda mchache mpaka mchanganyiko upate moto kidogo.
Baada ya hapo, paka kwenye kucha zako kwa kutumia pamba, fanya hivyo kabla hujapanda kitandani, ukimaliza vaa gloves kisha acha mpaka asubuhi, ukiamka zisugue kucha zako kisha zioshe.
Hapo shoga yangu utashuhudia mng’aro wa ajabu wa kucha zako, upo?

Leave A Reply