The House of Favourite Newspapers

Tumia mizizi ya tangawizi kutibu vidonda koo

LEO kwenye ukurasa huu tutaona jinsi ya kutibu vidonda koo kwa kutumia tangawizi na limao kwa kuanza tuanze na maji ya limao.

Maji ya limao ni mazuri kwa sababu yana vitamin C ambapo inasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kuponya tatizo hilo.

 

Kama unasumbuliwa na vidonda koo chukua maji ya limao changanya na maji kiasi, chumvi na asali au unaweza kutumia chumvi tu badala ya asali ukapona kabisa lakini kama unaweza kuchanganya vyote kwa pamoja ni vizuri zaidi.

Maji haya kunywa asubuhi, mchana na jioni utaona jinsi utakavyopona haraka.

 

Chai ya mizizi ya tangawizi

Chai ya mizizi ya tangawizi ina uwezo wa kuua bakteria kwa sababu yenyewe ni anti-bacterial na ina uwezo wa kukutibu kabisa tatizo hilo.

 

Jinsi ya kuandaa chai hiyo kama tiba

Vinavyohitajika ni mizizi ya tangawizi

Maji lita moja .

Kijiko 1 cha asali.

Limao kipande na maganda yake

 

Jinsi ya kuandaa

Osha mizizi kisha itwange iweke kwenye bakuli.

Chemsha maji kwenye sufuria.

Baada ya hapo weka kijiko kimoja kilichopondwa kwenye maji acha kwa muda wa dakika 10.

Baada ya hapo weka limao zima kipande na asali vyote kwa pamoja.

Chai hii unaweza kuinywa ya moto au ya baridi vyote vinatibu vizuri tu.

Mbali na kutibu madonda lakini pia chai hii ya mizizi ya tangawizi inasaidia kuondoa kabisa maambukizi.

Tiba hii imeombwa na Aisha wa Dar ambaye anasumbuliwa na vidonda koo mara kwa mara.

MWIGULU HOI KITANDANI: “NIOMBEENI TU, NAUMIA KIUNONI”

Comments are closed.