Tumia parachichi baada ya kunyoa ndevu

avokádoTatizo la kutoka vipele baada ya kunyoa ndevu au sehemu nyingine limekuwa likiwakumba wengi. Hata hivyo, leo nitazungumzia namna unavyoweza kukabiliana na tatizo hilo baada ya kunyoa ndevu kwa wanaume na wanawake pia.

Tunda la parachichi au mafuta yake ni mazuri kwa tatizo hilo. Tumekuwa tukijua tu kwamba linaweza kutibu chunusi lakini leo nataka nikueleze jinsi tunda hilo linavyopambana na vipele kidevuni au sehemu nyingine ya mwili.

avocado-sliced-in-halfJinsi ya kufanya

Chukua mafuta ya parachichi, paka kwenye ndevu kabla hujanyoa, paka mpaka ndevu ziloe kisha anza kunyoa.

Parachichi fresh

Lichukue ulimenye kisha lipondeponde vizuri, ukishanyoa unaweza kupaka kama after shave. Baada ya kupaka kaa kwa muda wa dakika 30 kisha osha.

Mafuta yake yanasaidia kukuacha mwili unatelezea na pia si rahisi kupata mapele au kuumiza ngozi wakati unanyoa.

Ni nzuri kwa kuilinda ngozi na siku zote ukiamua kutumia njia hii hutapata mapele. Siyo lazima kutumia njia zote, unaweza kutumia njia moja lakini pia ukitumia zote si mbaya.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
GLOBALBREAKINGNEWS.JPG


Loading...

Toa comment