The House of Favourite Newspapers

Tunakosea Kumlinganisha Young Killer na Young Lunya

0

IMEKUWA ni jambo jema sasa kwa mashabiki wengi na vyombo vya habari hususan redio na televisheni huwa wanajaribu kuwalinganisha wasanii wawili wanaofanya poa kunako anga la muziki wa Hip Hop, Young Lunya na Young Killer.

Huko kwenye mitandao ya kijamii ndio usiseme. Watu mapovu yanawatoka kwamba eti Young Lunya anamkosesha usingizi Killer, wengine wanathubutu kusema eti bwa’mdogo huyo amemzidi kabisa Killer. Na wengine wanafika mbali zaidi kiasi cha kunena kuwa Young Lunya ni bora kuliko Young Killer (fedheha jamani).

Ulinganisho wao umefanya nipate swali kuu la kuwa; “Wanatumia vigezo gani katika kuweka linganisho?” Maana katika kweli yenye kweli kuna mambo makuu matano katika kuwaweka watu kwenye mizani kama kweli unataka kufanya mambo kitaalamu.

Makala haya yanakuchambulia mambo hayo ya muhimu ambapo mwisho wa siku utabaini kwamba ni kosa kubwa sana kumlinganisha Young Lunya na Young Killer:

MOSI; ‘RAP SKILLS’

Hapa tunatazama uwezo wa msanii husika katika upana wa utunzi wa mashairi. Je, ana kiwango cha juu? Na uwezo wa kubadilika upo na upana? Je, katika rap skills unaweza kumuweka Lunya na Killer? Thubutu!

MBILI; CONSISTENCY

Uwezo wa kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu tangu kufahamika kwake. Lakini ubora wa kazi na nidhamu. Je! Lunya amedumu vipi? Ila nidhamu yake ya kazi mnaijua?

Na tukitaja wasanii 20 bora wa Hip Hop, Lunya anaweza kuwepo? Uhalisia ni Killer yupo katika muda mrefu tangu alipoanza kujulikana mpaka sasa.

TATU; ‘BODY OF WORK’

Katika mwili wa kazi tunatazama msanii tangu atoke ana album ngapi? Je! EP? Au kanda mseto? Ilihali ana nyimbo au video ngapi ambazo zimewahi kufanya vyema?

Sasa linganisho la Lunya na Killer linatoka wapi? Ikiwa tu Lunya hana hata wimbo mmoja ambao umewahi kuwa katika chati yoyote ya muziki.

NNE; ‘CULTURE IMPACT’

Mtazamo mkuu hapa ni msanii amefanya nini ambacho kimeleta mapinduzi katika uwanja wa muziki? Je! Uhalisia kati ya Lunya na Killer nani amefanya mapinduzi? Nani amegusa jamii katika mengi yenye mengi? Kwa upana wa kukumbukwa katika mengi zaidi? Ni wazi ni Young Killer, hili halina ubishi, bali wabishi kutaka kuleta ubishi kwa ubishi usio ubishi kabisa.

TANO; ‘ACCOLADES’

Hii ni sifa ya tuzo haswa, ambapo ni tuzo ngapi msanii husika amewahi kupata katika sanaa yake? Katika uhalisia wa vigezo vikuu vitano, ni kosa na makosa kwa watu kumfananisha Young Killer na Young Lunya. Haipaswi kuwepo kwa mfanano kabisa.

Killer ana Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop anayechipukia ya Kilimanjaro 2014, Lunya ana nini? Tuheshimu nafasi ya Young Killer katika muziki huu, lakini uchipukizi wa Lunya pia tunaufurahia, kuanza kumlinganisha na wakubwa zake ni kumvisha vazi lisilomtosh

Leave A Reply