The House of Favourite Newspapers

Tunda Amnanga Calisa

tunda-211Stori: MAYASA MARIWATA | Gazeti la Amani Toleo la Desemba 22, 2016

VIDEO queen machachari Bongo, Tunda Sebastian amemnanga vikali mwanamitindo maarufu ambaye siku chache zilizopita alihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa filamu Wema Sepetu, anayejulikana kwa jina la Calisa na kudai kuwa mwanaume huyo hana sifa za kuwa naye kimapenzi.

calisah-5Calisa

Akibonga machache na paparazi wetu bishosti huyo kutokana na kuulizwa madai ya kuwa kipindi cha nyuma aliwahi kubanjuka na Calisa, alifunguka kuwa ishu hiyo haijawahi kutokea na ni vigumu kutokea sababu hajawahi kuvutiwa naye na wala hana sifa za mwanaume anayemhitaji.

“Yani nilishangaa kusikia watu wanasema nimetembea na Calisa, hizo ni ndoto na hazitotimia, nikuhakikishie haitatokea kamwe ukasikia tumekuwa wapenzi, huyo kaka hana sifa hata moja ya kuwa na mimi, hanivutii hata kidogo,”alisema.

Comments are closed.