TUNDA ANG’AKA KUMWAGANA NA WHOZU

VIDEO Vixen Bongo, Ana Kimario ‘Tunda’ amesema anashangaa kuona watu wakimnanga kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mpenzi wake wa sasa Whozu wakati si kweli. Akizungumza na Amani, Tunda alisema Wabongo siku zote wamekuwa na mawazo hasi tu badala ya kuwawazia mazuri.

“Nashangaa watu wanasema kuwa mimi nimeachana na Whozu, yaani wanapenda kuniombea mabaya tu, siku nyingine wawe wananiombea heri basi. Sasa niwapashe tu, sijaachana na Whozu na sitarajii kuachana naye, watasubiri sana kwa hili,” alisema Tunda.

Stori: Neema Adrian


Toa comment