The House of Favourite Newspapers

Tunda Awaka Kuitwa Chuma Ulete

VIDEO vixen asiyeishiwa habari Bongo, Tunda Sebastian amewaka ile mbaya na kuhoji kwa nini watu wanamuita chuma ulete kwani ni jina geni kwake na linatokana na ushirikina kwenye biashara.

 

Tunda anayependa kujiachia kwenye hoteli za kifahari ameiambia Over Ze Weekend kuwa, anashangazwa na ishu hiyo kwa sababu kama ishu ni kula bata hotelini, hayo ni maisha yake.

 

“Mimi chuma ulete? Kivipi? Kama ishu ni kuishi hotelini, hayo ni maisha yangu, hebu watu waniache pliiz,” amesema Tunda dizaini kama amepaniki f’lani hivi.

STORI: IMELDA MTEMA

Comments are closed.