Tunda hata akifa ghafla hana kinyongo na mtu

Tunda Sebastian

MAKUBWA! Muuza nyago matata Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kuwa, hata kama atakufa leo hii, hana kinyongo na mtu yeyote.

 

Tunda ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, hakuna asichokipenda kama kukaa na kitu moyoni bila faida yoyote hivyo kama mtu anamkosea atamwambia na hapohapo anamsamehe kabisa.

 

“Hata nikifa ghafla leo hii, sina kinyongo na mtu yeyote kwa sababu vinyongo havina nafasi kwenye moyo wangu, wakati wote ni amani tu,” alisema Tunda ambaye amekuwa akikwaruzana na rafiki zake kutokana na skendo ya kuwakwapulia mabwana zao.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment