TUNDA: KUISHI HOTELINI MBONA POA TU!

Anna Kimario ‘Tunda’

VIDEO Vixen maarufu Bongo kwenye video za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anna Kimario ‘Tunda’ amesema kukaa kwake hotelini kila mara ni kitu cha kawaida, huku akidai kuwa siyo kwamba hana fedha za kulipa kodi ya nyumba.  Tunda alisema kuwa, watu wengi wanachonga sana kwa kitendo chake cha kuishi hotelini lakini hawajui siri ya yeye kwenda sana huko kuwa ni kupumzika na kubadilisha mazingira.

“Yaani watu hawajui kubadilisha mazingira kunasaidia hata kupanuka kwa akili na kupoteza mawazo, lakini wengine wanajisemea tu, eti Tunda ameishiwa hela ya kodi. Sasa wajiulize, kodi ya hoteli na nyumba ni ipi kubwa? Waache kuchonga, mimi natuliza kichwa changu baada ya kazi nyingi,” alisema Tunda

 


Loading...

Toa comment