The House of Favourite Newspapers

Tunda, Bella Kupanda Jukwaa Moja

 MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Tunda Sebastian anatarajiwa kupendezesha usiku wa King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ utakaofanyika Novemba 30, mwaka huu ndani ya Meeda, Sinza jijini Dar.

 

Katika usiku huo utakaoanza saa mbili za usiku, Tunda atapendezesha kwa kupanda jukwaani na kuwapa ‘hi’ mashabiki wote watakaojitokeza kwa wingi.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Bella ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Marekani katika ziara ya kimuziki alisema kuwa, amedhamiria kupiga shoo mfululizo na kwa kuanza ataanzia Ukumbi wa Meeda kisha atamalizia Sikukuu ya Krismasi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

“Mashabiki wana hamu ya kuiona Malaika Band na Christian Bella na hii itakata kiu yao kwani ni mwendo wa shoo baada ya shoo. Tukutane Meeda Novemba 30, kwa kiingilio cha elfu 10,000 tu,” alisema Bella.

 

Bella anatamba na nyimbo nyingi kama Msaliti, Nakuhitaji, Nashindwa, Rudi, Pambe na Punguza Mikogo.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

Comments are closed.