The House of Favourite Newspapers

TUNDA KUWA MC SHOO YA BELLA

Anna Kimario ‘Tunda’

MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Anna Kimario ‘Tunda’ anatarajiwa kuwa mshereheshaji katika shoo baab’kubwa ya King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ itakayofanyika Novemba 30, mwaka huu ndani ya Meeda, Sinza jijini Dar.  Akizungumza na Ijumaa, Bella anayekimbiza na ngoma kibao akiwa na bendi yake ya Malaika alisema katika usiku huo, kwa mara ya kwanza Tunda ataweka historia ya kuwa MC kwani hajawahi kufanya hivyo tangu ameingia kwenye muziki.

“Hii ni kwa wapenda burudani wote, usiku huu utapendezeshwa na Tunda ambaye kweli itakuwa balaa mwanzo mwisho. Unajua nimegundua mashabiki wana hamu ya kuiona Malaika Band ikiwa na Christian Bella na hii itakata kiu yao. Tukutane Meeda Novemba 30, kwa kiingilio cha elfu 10 tu,” alisema Bella.

Baada ya shoo hiyo, Bella anatarajiwa kufunika ‘bovu’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi akiwa na Malaika ambapo watapiga ngoma zao zote kuanzia Msaliti, Nakuhitaji, Nashindwa, Rudi, Pambe hadi Punguza Mikogo

Comments are closed.