Tunda na Penzi La Mbunge, Mh!

 

Tunda Sebastian.

BAADA ya Dishi Bovu kunasa ubuyu kwamba mwanadada, Tunda Sebastian kuwa anatoka na mbunge mmoja hivi anayemiliki hoteli ya kifahari jijini Dar na kumpangishia ‘apartment’ maeneo ya Tegeta, liliamua kutega antena zake ili kuweza kunasa kinachoendelea baina ya Tunda na mbunge huyo ambaye anawekwa kwenye mabano kwa kipindi hiki!

 

Dishi Bovu kwa kuanza liliwachokonoa watu wa karibu wa mwanadada huyo ili waweze kuunguza picha ambapo baada ya kumpata shoga yake mmoja mzurimzuri ambaye huonekana na Tunda mara kwa mara kwenye sherehe za kiburudani (hakupenda tummulike tochi) hivi ndivyo alivyofunguka; Shoga Mtu: Aaah! Kwani Tunda hata akiwa na mbunge au waziri kuna tatizo gani? Dishi Bovu: Tunataka tu ututhibitishie, hata sisi tunajua hakuna tatizo!

Shoga Mtu: Sasa niwathibitishie vipi? Niwatumie picha wakiwa faragha?

Dishi Bovu: Kama inawezekana, tena hapo utakuwa umesafisha picha haswaa! Shoga Mtu: Haa haaa! Siwezi kufanya huo ujinga ingawa ninafahamu kwamba ni kweli Tunda yupo na mbunge, ila mtafuteni mwenyewe, si namba yake mnayo. (Twiiii…shoga huyo aliminya kitufe chekundu cha simu yake, ikakatika.)

Dishi Bovu huyoo sambamba na Tunda Baada ya Dishi Bovu kuchonga na Shoga Mtu halikupenda kuacha ‘network’ ikisachi mchelemchele, liliamua kumtafuta Tunda ili aweze kufunguka ukweli wa madai hayo.

Dishi Bovu: Tundaa… Tunda: Nambie!

 

Dishi Bovu: Hongera mamaa!

 

Tunda: Kwa lipi? Kwanza naongea na nani mwenzangu?

Dishi Bovu: Ahaaa Tundaaaa!

Dishi Bovu hapa! Tunda: Shida yako?

Dishi Bovu: Nakuona unawakimbiza wenzio mjini!

Tunda: Kina nani?

Dishi Bovu: Mastaa wenzako! Tena huyo mbunge ambaye mna-share shuka eti amekupangishia apartment Tegeta siyo?

Tunda: Simjui bhana huyo mtu unayemzungumzia. (Twiii…naye alikata simu. Ingawa alipigiwa mara kadhaa hakuweza kupokea kabisa.)

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment