Tunda: Sidangi, Corona Haijanizuia Kula Bata

MTOTO wa mjini ambaye jina lake halisi ni Anna Kimario ‘Tunda’ amekuwa kimya, wambea wameanza kuibua maneno oooh, anaishije kipindi hiki cha Corona na alikuwa akitegemea kudanga?

Kwenye mahojiano maalum na Risasi Mchanganyiko, Tunda ameeleza wazi kuwa yeye haishi kwa kutegemea kudanga kama wengi wanavyodhani.

 

Amefafanua mengi kuhusu ukimya wake wa sasa kwenye ukurasa wake wa Instagram, karibu tujiunge naye hapa:

Risasi: Umekuwa kimya sana kwa hivi sasa, nini tatizo?

Tunda: Kuwa kimya kuna maana nyingi sana, kukaa na kutafakari mambo yako mengi au kuna sehemu unataka ubadilishe, maisha yako tofauti na yalivyokuwa huko nyuma.

 

Risasi: Lakini hata kwenye mitandao umekauka sio kama zamani!

Tunda: Ninachoamini kila mwanadamu ana nyakati zake za kufanya mambo yake, kuna wakati yale mambo yanashamiri na wakati mwingine yanapotea kabisa ndio hivyo, na huwezi juwa kuwa yanaweza kuibuka tena.

 

Risasi: Inaonekana kuwa labda huu ugonjwa wa Corona, umeleta mabadiliko maana hata zile picha za mahotelini hakuna.

Tunda: Ndio maana nikakwambia kuwa kila kitu kina muda wake na hata huo ugonjwa huujaleta chochote kwa sababu kuna magonjwa mengine kabla ya hili na mambo yalikuwa yanaendelea.

 

Risasi: Hivi haya madai ya kusema kuwa ulikuwa unadanga lakini sasa hivi hali ya huu ugonjwa itakuwa imekufanya utulie, vipi hilo?

Tunda: Hivi hayo mambo ya kudanga yanatokaga wapi, ina maana watu wasione mtu ana maisha mazuri anadanga, kweli jamani? Sio sawa hata kidogo na pia wakumbuke kuwa hata sisi tuna wazazi na wana uwezo wao wa kutufanyia kila kitu tofauti na wanavyofikiria.

 

Risasi: Mara kwa mara ulikuwa ukimposti picha mpenzi wako Whozu japokuwa najua mlikuwa na tofauti na mkazimaliza, vipi sasa hivi kuna shida gani?

Tunda: Kila kitu kina muda na wasaa wake, na hata sasa kwenye ukurasa wangu wa Insta siposti vitu vya ajabu, nimeamua kubadili maisha yangu na pia nimejifunza sio kila mpenzi wa kumposti.

 

Risasi: Kuna kipindi nilionaga umeposti picha kwenye mtandao wako wa Instagram uko nyumbani kwenu Arusha na watu wakadai umerudi kwenu jiji limekushinda, ni kweli?

Tunda: Mkataa kwao siku zote ni mtumwa kabisa, mimi hata nikirudi nyumbani nafurahi tu sana kwa sababu ni kwetu siulizwi na mtu na pia wajue ndio sehemu naipenda kuliko chochote.

 

Risasi: Vipi kuhusu kuishi hotelini?

Tunda: Kila mtu ana jinsi ya kuishi kwenye maisha yake, hivyo yasikupe kazi kutafakari ya mwenzako na wakati yako unayo mengi tu.

Risasi: Kwa hiyo, sasa hivi unajishughulisha na nini?

 

Tunda: Sidhani kama ni vyema kila mtu ajue ninachofanya, sio kila anayekuangalia kwa jicho ni mwema, hivyo tu!

Risasi: Wasichana wengi wa rika lako tayari wana watoto, vipi wewe nini tatizo?

Tunda: Mimi bado na sio kwamba wakipata na mimi nifuate mkumbo hapana, nitazaa kwa wakati wangu sahihi.

Risasi: Haya shukurani sana Tunda.

Tunda: Asante sana.

MAKALA: IMELDA MTEMA


Toa comment