The House of Favourite Newspapers

Tunda, Whozu Utamu wa Penzi Umefika Penyewe

0

VIDEO Vixen Bongo, Anna Kimario ‘Tunda’ amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kutimiza mwaka mmoja wa uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake Whozu na kusema kwake anaona ni kama miaka kumi.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Tunda amesema kuwa mara nyingi anakutana na watu ambao sio sahihi, hivyo hata wakiachana anaonekana yeye ndiyo tatizo kumbe wakorofi ni wanaume.

 

“Namshukuru sana Mungu, mwaka mmoja tumetimiza lakini watu wanaweza kuona ni mdogo, lakini kwangu ni mkubwa mno kwa vile sipendagi kuchukua muda na mtu ambaye angenisumbua akili yangu hata siku moja,” alisema Tunda ambaye pia amewahi kuwa na mahusiano tofautitofauti kabla ya kuwa na Whozu akiwemo Mtangazaji Casto Dickson.

STORI: IMELDA MTEMA

USIYOYAJUA KUHUSU MASHUJAA HAWA, RUGE, MUFURUKI, MENGI..

Leave A Reply