Tupo Mtaani Kwako ya ACB Bank Yazinduliwa
Kampeni mpya ya Tupo Mtaani iliyoletwa na Benki ya ACB imekuwa gumza. Hiyo ni baada ya Benki ya ACB kuzindua rasmi rasmi program ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo.
“Sasa tunakufikia popote ulipo kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.
Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la DSM.