The House of Favourite Newspapers

Kwa Hili ‘TUSI’ la Zari kwa Diamond, Wamefika Pabaya

MJASIRIAMALI maarufu Afrika Mashariki na Kati, Zarina Hassan maarufu kwa jina la Zari The Bossy Lady,  ameibua maswali baada ya kumu-wish heri ya siku ya kuzaliwa baba watoto wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari ameweka picha ya watoto aliozaa na Diamond ambao ni Tiffah na Nillan na kuandika; “Happy birthday mwenye vikima vyake.”

Dongo hilo limekuwa likitumika sana siku za hivi karibuni lakini kwa uhalisia kima ni aina ya mnyama anayeishi porini na ni jamii moja na tumbili, nyani na ngedere lakini haijafahamika iwapo kima aliokuwa anawamaanisha Zari ni mademu wa Diamond ama watoto wake.

 

Baadhi ya mashabiki  wamemgeuzia kibao wakisema iwapo Diamond ni mwenye vikima basi Zari ni mama vikima,  huku wengine wakimtetea na kusema ametumia maneno ya utani wala hakumaanisha hkama wanavyodhani.

WEMA amejibu maswali yote Uliyokuwa Unajiuliza!!

Comments are closed.