Tusua Maisha: Marry Mwalingo Akabidhiwa Dinner Set, Mbeya – Video

MWANAMAMA Marry Mwalingo aliyeibuka mshindi wa dinner set katika droo ya nne ya Promosheni  ya Tusua Maisha na Global inayoendeshwa na Kampuni ya kuchapisha Magazeti ya Global Publishers kila wiki.

 

Bi. Marry ambaye ni miongoni mwa washindi wanne wa Tusua Maisha na Global wiki ya nne, alikabidhiwa zawadi hiyo juzi Alhamisi, Agosti 9, 2018 na Wakala wa Global Publisher, Mkoa wa Mbeya, Mohamed Lalika katika ofisi zake zilizopo jijini Mbeya.

 

Aidha, akipokea zawadi hiyo Bi. Mwalingo alisema ushindi wa zawadi hiyo imekuwa ni chachu kubwa ya kuweza kuendelea na promosheni hiyo huku baadhi ya wadau wa Magazeti hayo wameeleza kutiwa moyo baada ya mshindi huyo ambapo kila Jumanne saa 10:00, droo hiyo huchezeshwa na kurushwa Live kupitia Global TV Online kisha washindi wanne hukabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki mpya, ada ya shule, dinner set na jezi mpya za soka.

 

Kushinda ni rahisi, nunua gazeti lolote la Global Publishers  ambayo ni Uwazi, Amani, Ijumaa,  Ijumaa Wikienda,  Risasi Mchanganyiko, Risasi Jumamosi, Championi na Spoti Xtra kisha fuata maelekezo ukurasa wa pili. Hujachelewa bado, nunua sasa utusue maisha kilaini.

Tusua Maisha: Bi. Mwalingo Akabidhiwa Dinner Set, Mbeya

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment