Tusua Maisha: Meneja Global Aanika Washiriki Wanavyoshinda Pikipiki

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho, akiwafafanulia wahariri kuhusu ripoti ya Shindano la Tusua Maisha na Global  lililofikisha wiki ya tatu.

 

MENEJA Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers,  wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, Abdallah Mrisho,  amesema maendeleo ya shindano kabambe linaloendeshwa na Kampuni hiyo la Tusua Maisha na Global linaendelea vizuri na wasomaji wa magazeti hayo wamekuwa na mwamko mkubwa wa kushiriki.

Wahariri na viongozi wakifuatilia ripoti hiyo.

 

Akizungumza wakati akiwasilisha Ripoti Maalum kwa Bodi ya Wahariri, Idara ya Usambazaji na Viongozi wa Idara zote za kampuni hiyo, Mrisho amesema droo tatu zimeshachezeshwa tangu kuanza kwa shindano hilo Juni 15, 2018 na washiriki 12 wameibuka washindi wakiwemo watatu wa pikipiki, wengine wa vyombo vya maakuli (dinner sets), headphones za Beats by Dre na jezi za Kombe la Dunia.

kutoka kushoto ni mhariri msaidizi wa Gazeti la Spoti Xtra, Samson Mfalila, Mhariri wa Championi, John Joseph na Mkuu wa Idara ya IT, Edwin Lindege,  wakifuatilia ripoti hiyo.

Aidha, Mrisho amesema mfumo wa kushiriki katika shindano hilo, na uchezeshwaji wa droo ni wa wazi na wa makini zaidi kwani unatumia mfumo maalum wa kiteknolojia ambao unachezesha droo na kutoa mshindi, hivyo hakuna mkono wa mtu wala kupangwa kwa mshindi.

 

“Kama mnavyoona ndugu wahariri na viongozi, mfumo wetu ni wa wazi kabisa, mfumo wa kiteknolojia ambao unapokea ujumbe kutoka kwa wanunuzi wa magazeti yetu, kuchezesha droo na kutoa mshindi. Hivyo niwasisitize wasomaji wetu washiriki zaidi na zaidi kwani yeyote anaweza kuibuka mshindi kupitia Tsh. 800 yake au Tsh. 1,000 atakayonunua gazeti letu na kushiriki,” alisema Mrisho.

 

Kutoka kushoto (mbele) ni mhariri wa Spoti Xtra, Michael Momburi, Mhariri wa Amani, Erick Evarist na Mhariri Kiongozi, Amran Kaima.

 

Aidha, wahariri na viongozi wengine wakichangia ripoti hiyo walisema kuna baadhi ya mapungufu kidogo ikiwemo uelewa wa watu kuhusu namna na kushiriki kwani wachache wao wamekuwa wakikosea kutuma ujumbe baada ya kununua magazeti hayo.

 

Kutoka kushoto ni wahariri waandamizi, Richard Manyota, Mwalimu na Elvan Stambuli.

 

Hata hivyo, viongozi na wahariri wa Global Publishers walikubaliana kuendelea kuwahamasisha wasomaji wa magazeti yake pamoja na kuwapa elimu ya jinsi ya kushiriki ili kuboresha shindano hilo na kuwarahisishia kufahamu jinsi  wanavyoweza kushiriki na kuibuka washindi wa pikipiki.

 

Edwin Lindege akifafanua jambo wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo.

 

Global Publishers inaendesha shindano la #TusuaMaishaNaGlobal, ambapo zawadi kibao zikiwemo pikipiki, dinner sets, headphones za Beats by Dre, jezi za Kombe la Dunia 2018, ada ya shule za watoto na nyingine nyingi.

 

 

Mshiriki anatakiwa kununua gazeti lolote la Global Pulishers yaani; #Uwazi, #Amani, #Ijumaa,  #IjumaaWikienda,  #RisasiMchanganyiko,  #RisasiJumamosi,  #Championi, #SpotiXtra kisha kufuata maelekezo yaliyopo kwenye kuponi maalum ukurasa wa pili.

 

 

Maelezo kwa mshairiki ni: Nenda sehemu ya kutuma ujumbe (SMS), kwenye simu yako, andika namba  zilizopo kwenye kuponi ukurasa wa pili wa gazeti husika, kisha utatuma namba hizo kwenda namba 0719 386 533. (Hakikisha una salio au bando la kutuma meseji kwa kiwango cha kawaida tu).

 

Kisha jaza taarifa zako binafsi kwenye kuponi hiyo na tunza nakala ya gazeti lako kwani litahitajika wakati wa kuchukua zawadi yako. Kwa kutuma ujumbe, moja kwa moja unakuwa umengia kwenye kinyang’anyiro cha kujishindia  zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine zitakazotolewa kila wiki.

 

Washindi wa tusua Maisha na Global wiki ya kwanza wakiwa kwenye picha baada ya kukabidhiwa zawadi zao wiki iliyopita.

 

Namba yako itaingizwa kwenye droo itakayochezeshwa kila Jumamosi na kuonyeshwa moja kwa moja mtandaoni na Global TV Online. Utapigiwa simu iwapo utafanikiwa kujishindia zawadi yoyote kwa wiki husika. Kwenye gazeti kutakuwa na kuponi yenye taarifa zifuatazo; Jina kamili, namba ya simu, umri na mahali unapoishi.

 

 

Hata hivyo, msomaji anatakiwa kufahamu kuwa ili ithibitike kuwa yeye ndiye mshindi anatakiwa kutumia namba ya simu  iliyosajiliwa kwa jina lake, anatakiwa kuwa na kuponi iliyomfanya awe mshindi wakati wa kwenda kuchukua zawadi yake. Kama jina lililosajiliwa kwenye simu litakuwa tofauti na jina la mtumiaji, basi hatapewa zawadi husika.

 

Zingatia haya: Global Publishers inapenda kuwataarifu wasomaji wake kuwa gazeti moja litatumika kwa SMS moja tu (mtu mmoja tu kwa gazeti moja) na siyo vinginevyo. Kumbuka kushiriki kwanza na kujaza kuponi kwenye gazeti lako kabla hujampatia mtu mwingine kulisoma.

 

Picha na Richard Bukos | Global Publishers

 

TUSUA MAISHA NA GLOBAL: Droo ya Wiki ya Tatu

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment