WASHINDI WA DROO YA SABA NA NANE WAKABIDHIWA ZAWADI

Hatimaye washindi wa droo ya saba na nane kwenye Shindano la Tusua Maisha na Global, leo wamekabidhiwa zawadi zao walizojishindia, tukio lililofanyika katika Ofisi za Global Publishers, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Waliokabidhiwa zawadi zao leo ni Said Katambo wa Nachingwea, Lindi aliyefunga safari mpaka jijini Dar es Salaam kufuata zawadi yake ya pikipiki, na Ezbon Bwire aliyemwakilisha ndugu yake, Jackson Bwire wa Ukerewe ambaye pia amejishindia pikipiki.

Wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Benard Kapembe aliyejishindia headphones na Boniphace Malick wa Bunju aliyejishindia dinner set.
Washindi wengine ambao zawadi zao zitatumwa kwa wawakilishi wetu wa mikoani, Nobert Benjamin wa Nyamagana, Mwanza aliyejishindia dinner set, Gasper Ndimbo wa Mkuranga aliyejishindia jezi na Ally Bakari wa Vikindu aliyejishindia jezi.

Wakati huohuo, washindi wa droo ya tisa wamepatikana katika droo iliyochezeshwa Ijumaa ambapo Simba Ramadhan, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa pikipiki mpya huku Anna Mbise, mfanyabiashara kutoka Arusha akijishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro akijishindia jezi.

Ili kuwa miongoni mwa washindi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi vigezo na masharti vinazigatiwa.




(PICHA: RICHARD BUKOS | GPL)


Comments are closed.