The House of Favourite Newspapers

Tuyisenge in, Carlinhos Out Yanga

0
Mnyarwanda Jacques Tuyisenge

USISHANGAE siku ukiona Yanga inamtambulisha straika mwenye nguvu na urafiki mkubwa na nyavu, Mnyarwanda Jacques Tuyisenge na kumtoa kwa mkopo staa wao kipenzi, Carlos Carlinhos.

 

Awali, Yanga ilidaiwa kumtaka Tuyisenge anayekipiga APR ya Rwanda kwenye dirisha kubwa wakati huo alikuwa ametoka kusitisha mkataba wake na Petro Luanda ya Angola lakini dili lilishindikana na wababe wa Jangwani wakamshusha Michael Sarpong.

 

Sasa kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi imezipata kutoka kwa mmoja wa mabosi wanaosimamia usajili pale Yanga ni kuwa, wameamua kurejea tena kujaribu kumsajili Tuyisenge ambaye ni rafiki wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na walicheza pamoja Gor Mahia ya Kenya.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, tayari viongozi wameanza mchakato wa kuwasiliana na APR ili waweze kupewa Tuyisenge ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket, mkataba wake unaisha Juni 30, 2022.

 

Inadaiwa kuwa, kama wakifanikisha dili hilo haraka kwenye usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, atakuja kuchukua nafasi ya Carlinhos ambaye watamuuza kwa mkopo.

 

“Tayari tumewasiliana nao viongozi wa APR na kama watakubaliana na ofa yetu kwa Tuyisenge basi kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na Carlinhos ambaye tutamuuza kwa mkopo ili tuweze kupata straika mwenye uwezo wa kupambana kama ilivyo kwake (Tuyisenge).“

 

Msimu huu tunatakiwa kupata ubingwa hivyo tunaweka nguvu kubwa katika kuhakikisha tunapata mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kama Tuyisenge, hivyo muda si mrefu tutajua matokeo ya ofa yetu hiyo kutoka APR,” kilisema chanzo hicho.

Carlinhos ambaye amejiunga na Yanga akitokea GD Interclube ya nchini kwao Angola, mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao mawili na asisti mbili kwenye ligi huku muda mwingi akiutumia nje ya uwanja kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, azungumzie ishu hiyo alisema: “Kwa sasa tupo kidijitali na mambo yetu ya usajili tunaweka kwenye mitandao yetu ya kijamii na siyo sehemu nyingine.

Musa Mateja, Dares Salaam

Leave A Reply