The House of Favourite Newspapers

Tuzo nusura imuangushe Richie

0

Imelda Mtema,

AMANI

Tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili Afrika Mashariki aliyoipata hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Single Mtambalike ‘Richie’ katika sherehe za utoaji Tuzo za African Magic Viewers Choice 2016, almanusura imuangushe chini kwa kiwewe.

Akipiga stori na Amani, Richie alisema hakuamini kama kweli alishinda tuzo ile na aliposikia akiitwa jina lake kitendo cha kuinuka tu, alijihisi kupepesuka lakini alijitahidi na kufika jukwaani.

“Jamani kwanza sikuamini ni mimi siku ya kwanza naanza kuonekana DSTV, tena nikiwa nanyakua tuzo, kweli nilipata kama mshtuko mkubwa sana kipindi natembea nilihisi kupepesuka nikaona kama nataka kudondoka nikajipa nguvu ya ajabu,” alisema Richie.

Tuzo hizo zilitolewa nchini Nigeria ambapo pia kwa Tanzania, staa mwingine wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliibuka na Tuzo ya Filamu Bora Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu).

Leave A Reply