Tuzo ya Clayton yamponza Ester

ester4Na Deogratius Mongela

KIHEREHERE! Msanii wa filamu Bongo, Ester Kiama hivi karibuni alijiponza baada ya kushambuliwa mtandaoni kisa kikiwa ni kumsifu muigizaji mwenzake wa kiume, Omary Clayton aliyeshinda tuzo ya kimataifa ijulikanayo kama California Online Viewers Choice.

Akipiga stori na gazeti hili, Ester alisema aliweka ujumbe na picha kwenye ukurasa wake wa Instagram kuipongeza filamu ya Dogo Masai kuchukua tuzo nje ya nchi sambamba na kumpongeza Omary, lakini kilichotibua hali ya hewa ni kupewa ‘makavu’ na wasanii wenzake kwa kuona anajipendekeza.

“Imeniuma sana yaani wasanii hatuna ushirikiano, niliamua kuposti picha kwa lengo zuri kwani wameipeperusha vema bendera yetu, kinyume chake nilipewa maneno makali ambayo sikuyatarajia maana najua sisi wasanii ni kitu kimoja,” alisema.


Loading...

Toa comment