The House of Favourite Newspapers

Tuzo za NEA… hawa ndiyo ‘wachawi’ wa Vee Money

0

vee moneyBONIPHACE NGUMIJE

NIGERIA Entertainment Awards (NEA) ni tuzo kubwa Nigeria ambazo zimeanzishwa mwaka 2006 jijini New York, Marekani ili kuwainua wasanii wa Nigeria na sehemu tofauti barani Afrika. Tuzo hizo mwaka huu zitafanyika Septemba 4, ambapo miongoni mwa wasanii wanaoziwania ni diva kutoka Bongo, Vannesa Mdee akiwa katika kipengele cha Best African Female Artist.

Katika kipengele hicho Vanessa Mdee ambaye ni msanii pekee anayeipeperusha bendera ya Bongo katika tuzo hizo anategemea kukutana na upinzani mkali kutoka kwa wasanii wafuatao ambao kwake ni kama ‘wachawi’ wake katika kutimiza lengo lake la kunyakua tuzo hizo.

EFYA-3Efya

Efya na MZ Vee (Ghana)

Efya ni mkali wa Muziki wa Soul na muigizaji kutoka Ghana. Jina lake kamili ni Jane Awindor, amepata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki nchini humo ambapo tangu mwaka 2011 mpaka sasa amefanikiwa kujizolea tuzo tofauti nane barani Afrika.

Mwanadada huyu pia anaelezwa kuwa kati ya wasanii ambao wanafanya kazi kwa ukaribu zaidi na jamii nchini Ghana ambapo kwa sasa ni balozi wa taasisi ya kusaidia watoto wenye matatizo ya Kiwewe (Trauma) na waishio mitaani iitwayo Awal Children Of The Future Found-ation.

Huku Efya akitajwa kumpa upinzani mkali Vee Money, msanii mwingine wa RnB kutoka nchini humo Vera Hamenoo- Kpeda ‘MZ Vee’ aliyeanza gemu miaka mitatu tu iliyopita lakini akiwa amejizolea tuzo nane mpaka sasa ikiwa ni pamoja na kushindania tuzo za BET mara mbili anatajwa kuwa mchawi mkubwa wa Vee Money kwenye tuzo hizo.

victoria-kimaniVictoria Kimani (Kenya)

Jina hili si geni kwa wafuatiliaji wa burudani Bongo. Ni la mwanamuziki raia wa Kenya aliyezaliwa nchini Marekani katika familia ya kichungaji na sasa ni mkazi wa Lagos, Nigeria anakofanyia kazi zake za muziki.

Victoria aliyetamba na Wimbo wa Protoko na Show, ambaye pia ni mdogo wake na rapa Simon Kimani ‘Bamboo’ naye ni mchawi mkubwa kwa V- Money katika tuzo hizi na anapewa nafasi ya kutwaa pia tuzo hiyo maana siku za hivi karibuni amejitengenezea wigo mkubwa wa mashabiki barani Afrika.

LiraLira (Sauz)

Lerato Molapo ‘Lira’ ni mwanamuziki wa Soul mwenye mafanikio makubwa Afrika Kusini. Mwanadada huyu aliyekuwa akifanya kazi kwa karibu na mwanamuziki mwenye heshima kubwa Afrika Miriam Makeba, mbali na kutwaa tuzo kedekede mwaka 2010 aliungana na wasanii Alicia Keys, Shakira, K’Naan na John Legend kuimba Wimbo wa Pata Pata kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini humo mwaka huo.

SheebahSheebah (Uganda)

Sheebah Ndiwanjawulo ‘Sheebah’ ni msanii anayepanda kwa kasi kutoka Uganda. Anatamba na Ngoma ya Sheebah Karungi na ni kati ya wasanii wanaotarajiwa kufanya vizuri kwenye Tasnia ya Muziki Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake.

Mbali na hao juu wanamuziki wengine ambao ni wachawi wa Vee Money kwenye tuzo hizo za Nea ni Adiouza kutoka Senegal na Knowless Butera kutoka Rwanda.

Leave A Reply