The House of Favourite Newspapers

TWANGA KUFANYA TAMASHA KUBWA KUFIKISHA MIAKA 20

Asha Baraka (katikati) akiongea katika mkutano huo. Kushoto ni Luiza Mbutu na kulia ni Kalala Junior.

Bendi ya African Stars Twanga Pepeta leo imefanya mkutano na wanahabari kuzungumzia tamasha lake la miaka 20 ya bendi hiyo. Akizungumza na wanahabari waliofikakwenye mkutano huo uliofanyika Legend Club Kinondoni jijini Dar, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu kwenye klabu hiyo.

Asha Baraka akimtambulisha Dogo Joshua ambaye ni tishio safu ya waimbaji.

Asha Baraka amesema kabla ya uzinduzi huo watafanya mambo ya kijamii ikiwemo kutoa misaada hospitalini na kwenye vituo vya watoto yatima.

Naye kiongozi wa wanamuziki wa bendi hiyo, Luiza Mbutu akizungumzia wasanii waliowahi kutamba na Twanga miaka ya nyuma kurudi kwenye bendi hiyo ambapo alisema si wote watakaokubaliwa.

Muimbaji wa Twanga zao la Bongo Star Search (BSS) Haji Ramadhani akifuatilia kiumakini mkutano huo.
Mapaparazi nao walikuwa kazini wakati mambo yakiendelea.
Asha Baraka akiwa na wanamuziki wake kwenye mkutano huo.
Luiza Mbutu akiwazungumzia wanamuziki waliotimka kwenye bendi na sasa hivi wanatamani kurejea.
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.