The House of Favourite Newspapers

Twanga, Msondo, Sikinde kuwasha moto Valentine’s Day Dar Live

0

IMG_5661 The African Stars ‘Twanga Pepeta,’

Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

WAKONGWE wa Muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta,’ Sikinde, Msondo Ngoma pamoja na kundi la muziki wa Taarab, TOT wanatarajiwa kuwasha moto Sikukuu ya Valentine’s Day (Feb 14) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

msondoMsondo Ngoma

Akizungumza na Mtandao huu Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo utakuwa ni usiku wa kukumbukwa kwa wapendanao kutokana na burudani zilizoandaliwa na bendi hizo ambazo ni kongwe nchini.

Mbizo aliongeza kuwa, usiku huo utakuwa wa aina yake kwa vijana na wazee wa zamani kutokana na bendi hizo kupiga nyimbo ambazo hazichuji na zinazopendwa kila zinaposikika masikioni mwa wapenda burudani.

s1Sikinde

“Utakuwa ni usiku wa kihistoria, njoo na mwandani wako muwashuhudie Twanga, Sikinde, Msondo Ngoma pamoja na TOT kwa kiingilio cha Sh. 20,000 kwa VIP na kawaida Sh. 10,000 tu,” alisema Mbizo.

Meneja huyo alisema ulinzi utakuwepo wa kutosha ndani na nje ya ukumbi hivyo watu waje na magari pamoja na pikipiki bila kuhofia usalama.

Aidha, aliahidi kila kapo itakayopendeza usiku huo itatoka na zawadi.

Leave A Reply