The House of Favourite Newspapers

Twanga Pepeta Yatambulisha Vibao Vipya

Mambo yakiendelea jukwaani.

BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kuamkia leo ilitambulisha nyimbo zake mpya kwa mashabiki kwenye onyesho maalum la ‘Listening Party’ lililofanyika Ufukwe wa Coco jijini Dar.

 

Ally Choki (kushoto) na Luiza Mbutu wakikamua.
Mwanamuziki Kalala Junior na mnenguaji Otilia Boniface wakionyeshana kazi.
Wanenguaji wa Twanga wakicheza kibao cha asili kiitwacho Kalunde.
Ally Choki na Luiza Mbutu wakimdatisha Mzungu.

Katika onyesho hilo mashabiki waliofurika ufukweni hapo walipata burudani ya vibao mbalimbali vya bendi hiyo kuanzia vilivyowahi kutamba enzi hizo. Vibao vipya vilivyotambulishwa mbele ya mashabiki ni Prison Love na Mapenzi ya Mwendokasi.

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

Comments are closed.