The House of Favourite Newspapers

Twiga Stars Kupindua Meza Kwa Namibia

0

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime, amesema walifanya makosa
kwenye mchezo uliopita
wakiwa nyumbani na sasa wanakwenda kuwafunga Namibia wakiwa kwao, kesho Jumamosi.


Twiga Stars walichapwa 2-1
na Namibia kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kwenda Afcon
mwakani, kwenye mtanange
uliochezwa juzi Jumatano Uwanja wa Mkapa, Dar.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, Shime alisema walifanya makosa kwenye mchezo uliopita, wameliona hilo na watakwenda kulifanyia kazi wakiwa ugenini ambako kwa namna yoyote lazima wapate ushindi.

Leave A Reply