The House of Favourite Newspapers

Twiga Stars: Tutashinda na Kufuzu Afcon

0

KOCHA Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime, amesema kuwa leo Jumamosi watafanya maajabu kwa kushinda
na kufuzu michuano ya
Afcon kwa wanawake mbele ya Namibia kwa kushinda mechi hiyo.

 

Twiga Stars watacheza na Namibia kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye mji wa Port Elizabeth, Afrika Kusini huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa 2-1 nyumbani.

 

Shime alisema: “Tupo kwenye uwanja wa vita na tumekuja kupambana kweli, haitakuwa rahisi lakini matumaini yetu ni kwamba tutashinda. Wenzetu wapo nyumbani na wana mtaji wa mabao mawili, itabidi tuupande mlima mrefu sana.”

Stori: Issa Liponda,Dar es Salaam

Leave A Reply