The House of Favourite Newspapers

Twiga Stars watembelea duka la kisasa la Airtel Expo Dar‏

0

Pic 1Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Juma Hassan akitoa maelezo ya jinsi ya kupata huduma mbalimbali za kisasa kwa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars walipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo liliko Morocco jijini Dar es Salaam

Pic 2Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakimfatilia kwa makini Afisa Afisa wa huduma kwa wateja wa Airtel, Bw Stephen Makongoro wakati alipokuwa akitoa maelezo ya huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Twiga Stars ilitembelea duka jipya la Airtel Expo lililopo jijini Dar es salaam

Pic 3

Baadhi Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakitumia vifaa mbalimbali pamoja na simu za kisasa zilizopo katika duka la Airtel Expo wakati timu hiyo ilipotembelea duka hilio Jana, akishuhudia ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Boaz

Pic 4

Kikosi kizima cha timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars pamoja na uongozi wa timu hiyo na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati timu hiyo ilipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo lililopo Morocco jijini Dar Es Salaam

PIc 5

Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akimkabithi Meneja wa Timu ya Twiga Stars , Furaha Francis Modem aina ya Airtel wingle inayounganisha watumiaji zaidi ya 10 na huduma ya Wifi itakayosaidia kikosi hicho kuunganishwa na huduma za intaneti wakati wote. Modemu hiyo ilikabidhiwa wakati Airtel ilipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo lililopo Morocco Jijini Dar es Saalam


Pic 6

Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba (nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars ambao wametokana na matunda ya mpango wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa Airtel Rising Stars.

Pic 7Baadhi Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakitumia simu zilizopo ndani ya duka la Airtel Expo kupiga selfie na kuona ubora wa simu hizo wakati walipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo liliko Morocco jijini Dar es Salaam

Pic 8Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akimkabithi simu mmoja ya wachezaji wa timu ya wanawake ya Twiga Stars , Maimuna Hamisi mara baada ya kujibu maswali juu ya huduma na bidhaa za Airtel kwa ufasaha.

Kikosi cha timu ya wanawake cha Twiga Stars , leo kimetembea duka jipya la Airtel lilipo Morocco jijini Dar es Saalam na kujionea huduma mbalimbali za kibunifu na zenye technologia za kisasa na kuunganishwa na huduma mbalimbali za Airtel

Akiongea wakati wa kupokea kikosi hicho Mkurugenzi wa kitengo cha Huduma kwa Wateja, Bi Adrianna Lyamba alisema “ leo tunajisikia furaha sana kuwa na timu ya wanawake ya Tanzania katika duka letu hili, Tunaamini huduma tunazozitoa za mawasiliano zitawasaidia wao pia katika shughuli zao za kila siku nah ii ndio sababu tumeonelea ni vyema kuwakaribisha ili wajionee huduma hizi za kibunifu zikiweko huduma za intaneti, Airtel Money, na nyingine nyingi.

Sambamba na huduma mbalimbali tunazozito tumeona ni vyema kuwapatia timu hii ya Taifa ya wanawake Modem mpya ya kisasa ya Airtel wingle itakayoweza kuwaunganisha hadi watumiaji 10 kwa wakati mmoja. Tunamini modem hii itawawezesha wachezaji hawa kuunganishwa na internet wakati wakiwa kambini na kupata mbili mbalimbali za mpira pia kwenye simu zao kupitia huduma ya Airtel intaneti

Tunatoa wito kwa wateja wetu na watanzania mmoja mmoja kwa makundi kutembelea duka letu na kujionea huduma bora za kisasa zinazotolewa dukani hapa

Kwa upande wake Kocha mkuu wa Twiga Stars, Nassra Mohamed alisema” Tunashukuru sana Airtel kwa kutupa upendeleo wa pekee, tumejifunza mengi kuhusu huduma na bidhaa za kibunifu ambazo zimetupa mwanya sisi kama wachezaji ni jinsi gani ya kuzitumia. Huduma hizi kama vile ya Airtel intaneti itatuwezesha kupata mafunzo kwa njia ya mtandao kwa hiyo hili kwetu ni habari njema na tunawashukuru sana Airtel kwa kutupatia Airtel wingle itakayotuunganisha kwenye huduma ya intaneti”

Leave A Reply