The House of Favourite Newspapers

Twite kuweka rekodi ya pekee Yanga SC

0

arton49463Mchezaji kiraka wa Yanga, Mnyarwanda.

MCHEZAJI kiraka wa Yanga, Mnyarwanda mwenye asili ya DR Congo, Mbuyu Twite anatarajia kuandika rekodi ya pekee kikosini hapo katika mechi dhidi ya Medeama ya Ghana, Julai 15 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Rekodi hiyo itawekwa ikiwa Twite atacheza katika mchezo huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam ambapo anatarajiwa kuwa kiungo mkabaji, ikiwa hivyo atakuwa amecheza nafasi tatu tofauti katika mechi tatu tofauti za michuano hiyo zilizopita.
Taarifa kutoka Yanga zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm anamuandaa Twite kucheza nafasi ya kiungo mkabaji wakati ambapo katika mechi mbili zilizopita za hatua ya makundi ya michuano hiyo alicheza nafasi ya beki wa kulia, kisha wa kushoto na sasa atakuwa katikati.
“Unakumbuka mechi dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, Twite alikuwa beki wa kulia, dhidi ya TP Mazembe alikuwa beki wa kushoto na sasa anatarajiwa kuwa namba sita,” alisema mtoa taarifa kutoka Yanga na kuongeza:
“Twite ana uwezo mkubwa wa kukaba ndiyo maana kocha anataka kumtumia kama namba sita.”
Katika mechi zilizopita Thabani Kamusoko ndiye aliyekuwa namba sita, ikiwa mabadiliko hayo yatafanyika, Kamusoko atasogezwa mbele kuwa namba nane kisha Haruna Niyonzima akisimama kuwa kiungo wa pembeni.
Gazeti hili lilipomuuliza Pluijm kuhusiana na suala hilo alisema: “Hivi sasa ni mapema mno kulizungumzia ila nakiandaa kikosi changu kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huo.”

Leave A Reply