The House of Favourite Newspapers

U.T.I janga lisilopewa kipaumbele-2

0

urinary-tract-infectionWIKI jana tulianza kulielezea tatizo la U.T.I (Urinary Tract Infections) na nieleza kuwa hili ni tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo ambalo huwasumbua watu wengi siku hizi.

Maambukizi hayo yanaweza kusababisha maumivu na kukosa raha. Pia nilieleza kuwa UTI ni ugonjwa ambao huwaathiri zaidi wanawake ukilinganisha na wanaume, na sababu kubwa ikiwa ni ya kimaumbile, ingawa kuna sababu nyingine kama kufanya ngono na historia ya kifamilia.

Pia nilieleza UTI husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao huingia katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu. Asilimia kubwa ya ugonjwa huu katika jamii husababishwa na bakteria ajulikanaye kama Escherichia coli (E Coli), pia asilimia ndogo yaweza kusababishwa na aina nyingine ya bakteria ajulikanaye kama Staphylococcus Saprophyticus.

Leo ningependa kukujuza pia watoto waweza kuathirika na ugonjwa huu wa UTI, hususan watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka miwili na watoto wa kiume wasiotahiriwa.

Dalili kuu kwa watoto wenye ugonjwa huu ni homa, ingawa vipimo huhitajika ili kuhakikisha uwepo wa ugonjwa. Wazee nao pia huweza kuathirika na ugonjwa huu.
Kama nilivyoelea awali kuwa maambukizi haya katika mfumo wa mkojo ndiyo kitaalamu huitwa U.T.I. Mfumo wa mkojo unahusisha sehemu kuu nne:-

•Figo (Kidney), ambazo ni ogani zilizo na umbo la punje za maharage na zinakuwa mbili na ukubwa wake ni kadirio la unavyokunja ngumi yako. Kazi ya figo ni kuchuja damu na matokeo yake ni mkojo unaotengenezwa na hutolewa kama uchafu mwilini.

•Mirija ya kutoka katika figo kwenda kwenye kibofu (Ureters), huwa ni miwili na hupeleka mkojo kwenda kwenye kibofu.
•Kibofu, kazi yake ni kukusanya na kuhifadhi mkojo unaotoka katika figo, mkojo hutolewa pale mtu anapoamua kukojoa.

•Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu (Urethra), huu ni mrija mmoja ambao hutoa mkojo nje mtu anapoamua kukojoa.
Ugonjwa huu ambao hauko katika kundi la magonjwa ya zinaa, lakini kufanya ngono wakati mwingine husababisha kuambukizwa kwa ugonjwa huu.
Dalili za U.T.I hutofautiana kulingana na sehemu ya njia ya mkojo iliyoathirika.

FIGO
-Kichefuchefu.
-Kutapika.
-Maumivu ya mgongo wa juu.
-Homa kali.
-Kutetemeka na kusikia baridi

KIBOFU
•Damu katika mkojo.
•Maumivu ya nyonga.
•Maumivu chini ya kitovu.
•Kukojoa mara kwa mara na kupata maumivu wakati wa kukojoa.

MRIJA WA KUTOA MKOJO KUTOKA KWENYE KIBOFU (URETHRA)
•Mkojo wa kuunguza wakati wa kukojoa (maumivu njia ya mkojo)
Siyo mara zote ambazo mtu hupata dalili za ugonjwa huu, lakini zinapotokea huwa ni kama ifuatavyo:- Kujisikia haja ya kukojoa mara kwa mara, kusikia maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara mkojo kidogo, mkojo wa rangi ya mawingu, mkojo mwekundu au pinki, pia wa rangi ya brauni, mkojo unaotoa harufu, maumivu ya nyonga kwa wanawake na maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wanaume.

Endapo utakuwa na dalili hizo zilizotajwa awali ni vyema kupata ushauri wa daktari.
Nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume. Unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply