The House of Favourite Newspapers

U.T.I janga lisilopewa kipaumbele-3

0

m_jpg120003faTULIANZA kupeana ufahamu juu ya maambukizi katika njia ya mkojo yaani U.T.I na tuliangalia chanzo na wiki jana tuliangalia dalili za ugonjwa huu.
Leo tutaangalia makundi mbalimbali ambayo yapo katika hatari ya kupata maambukizi haya.

Wagonjwa walioingiziwa mpira wa kusaidia kutoa mkojo (Catheter) huwa katika hatari kubwa ya kupata U.T.I. Hii inajumuisha wagonjwa waliolazwa, wenye matatizo ya magonjwa ya fahamu na hawawezi kutoa mkojo, pia wagonjwa waliopooza.

Wagonjwa walio na kinga ya mwili iliyoshuka, mfano wale wenye kisukari na magonjwa mengineyo yanayoshusha kinga ya mwili dhidi ya vijimelea vya magonjwa, wanakuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu.

Wagonjwa walioziba njia ya mkojo, hii inaweza kusababishwa na mawe ya kwenye figo na kukua kwa tezi dume kwa wanaume, hii husabisha mkojo wenye bakteria kushindwa kutoka na kusababisha maambukizi katika kibofu na figo.

Hitilafu katika njia ya mkojo inawezekana mtoto kuzaliwa na hitilafu hii ambayo husababisha mkojo kushindwa kutoka kwa urahisi na kuchochea maambukizi haya ya U.T.I.

Ukomo wa hedhi, hii ni kwa sababu homoni ya (Ostrogeni) hupungua na kusababisha mabadiliko katika njia ya mkojo.

Matumizi ya njia za uzazi wa mpango, ambayo vipandikizi huwekwa katika njia ya kizazi (Diaphragm).Yaweza pia kuchochea kupata maambukizi haya.

Kuwa katika umri wa matamanio ya kufanya ngono. Wanawake walio katika umri wa matamanio ya ngono wameonekana kuathirika zaidi ya wale wasio na matamanio ya ngono.

Kuwa mwanamke, wanawake wana mrija mfupi wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu ukilinganisha na wanaume. Kwa hiyo huwa ni rahisi kwa bakteria kufikia kibofu kwa wanawake, na kupata uambukizi.

Ugonjwa wa U.T.I unapotibiwa mapema, hupona kwa urahisi na hakuna madhara yoyote atakayopata mgonjwa.Lakini ugonjwa usipotibiwa na kuwa sugu, madhara huweza kutokea. Madhara haya ni kama kuharibika kabisa kwa figo endapo mgonjwa ataishi na ugonjwa kwa muda mrefu bila kutibiwa.

Athari hizi huwa ni zaidi kwa watoto ukilinganisha na watu wazima. Mwanamama mjamzito asiyetibiwa ugonjwa, anaweza kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo au aliye njiti.

Pia mkojo waweza kuchunguzwa katika maabara kuangalia uwepo wa chembechembe za seli nyeupe za damu, seli nyekundu za damu au hata uwepo wa bakteria.
Ni vyema mgonjwa anapotoa mkojo wa uchunguzi kuhakikisha mkojo huo hauingii vijimelea kutoka katika mazingira ya anapotolea mkojo huo.

Kamwe usitumie dawa bila ya kupata ushauri wa daktari na vipimo kuhakikisha aina ya ugonjwa. Baada ya vipimo onana na mtaalam kwa ajili ya dawa na ushauri kuhusu matumizi ya dawa.

Kwa kawaida dalili za ugonjwa hutoweka siku chache baada ya kuanza kutumia dawa, lakini hiyo siyo sababu ya kuacha kutumia dawa. Unaweza hitajika kutumia dawa zako kwa muda wa zaidi ya siku saba ili upone kabisa.

Tumia dozi nzima kama ulivyoelekezwa ili kuhakikisha maambukizi yanamalizika kabisa.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya wiki ijayo. Nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume, unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply