The House of Favourite Newspapers

U.T.I; janga lisilopewa kipaumbele-3

0

m_jpg120003faWiki iliyopita nilielezea tatizo la mirija kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo Ureters, huwa ni miwili na hupeleka mkojo kwenda kwenye kibofu.

Kibofu ambacho kazi yake ni kukusanya na kuhifadhi mkojo unaotoka katika figo, hutolewa pale mtu anapoamua kukojoa.

Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu (Urethra) huu ni mrija mmoja ambao hutoa mkojo nje mtu anapoamua kukojoa.

Ugonjwa huu ambao hauko katika kundi la magonjwa ya zinaa, lakini kufanya ngono wakati mwingine husababisha kuambukizwa kwa ugonjwa huu. Leo naendelea kuelezea dalili tofauti… Endelea…

Dalili za maambukizi ya UTI hutofautiana kulingana na sehemu husika ya njia ya mkojo iliyoathirika, utazigundua kwa kuona tofauti hizi:-
λ Figo.
λ Kichefuchefu.
λ Kutapika.

λ Maumivu ya mgongo wa juu.
λ Homa kali.
λ Kutetemeka na kusikia baridi.
λ Kibofu kuuma.
λ Damu katika mkojo.

λ Maumivu ya nyonga.
λ Maumivu chini ya kitovu.
λ Kukojoa mara kwa mara na kupata maumivu wakati wa kukojoa.
λ Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu (Urethra).

λ Mkojo wa kuunguza wakati wa kukojoa (maumivu njia ya mkojo).
Siyo mara zote ambazo mtu hupata dalili za ugonjwa huu, lakini zinapotokea huwa ni kama ifuatavyo:-

λ Kujisikia haja ya kukojoa mara kwa mara, kusikia maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara mkojo kidogo, mkojo wa rangi ya mawingu mawingu, mkojo mwekundu au pink, pia wa rangi ya brauni, mkojo unaotoa harufu, maumivu ya nyonga kwa wanawake na maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wanaume.

Endapo utakuwa na dalili hizo zilizotajwa awali ni vyema kupata ushauri wa daktari.
Nikukumbushe kuwa Sigwa herbal clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume, pia unaweza ukawatembelea katika vituo vyao mbalimbali vilivyopo nchi nzima.

Kwa maelezo na msaada zaidi usisite kupiga simu.
Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply