The House of Favourite Newspapers

UAE yatangaza ufadhili wa dola bilioni 30 kutafuta muarubaini wa mabadiliko ya hali ya hewa

0

Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amesema uhaba wa ufadhili umekuwa ni suala linalodumaza uchukuaji wa hatua kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kote duniani.

Rais wa UAE Sheikh Al Nahyan anasema: “Uhaba wa ufadhili siku zote umekuwa ni changamoto kubwa katika kusonga mbele kwa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni kwahiyo, nimeridhishwa na kuundwa kwa mfuko wa ufadhili wenye thamani ya dola bilioni 30. Ufadhili umepangwa kujaza mwanya katika ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka hatua zichukuliwe akisema “ishara mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa zinaonekana.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema:“Tuko maili kadhaa kufikia malengo ya Makubaliano ya Paris na dakika chache kuingia usiku wa manane kwa ajili ya kiwango cha digrii 1.5. lakini bado hatujachelewa. Tunaweza, mnaweza, kuzuia hii dunia isianguke na kuungua.”

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken aliwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Al Maktoum huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiaraby siku ya Ijumaa kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa COP28.

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Joe Biden hawatahudhuria mkutano huu wa COP, wiki kadhaa baada ya kutangaza makubaliano ya pamoja ya kupunguza utoaji hewa chafu ya methane.

Leave A Reply