The House of Favourite Newspapers

Ubalozi wa Palestina Nchini Tanzania Watoa Tamko Kufuatia Mauaji ya Mwandishi wa Habari

0
Shireen AbuAqla Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Al-Jazeera

UBALOZI wa Palestina nchini Tanzania umetoa tamko la kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa habari Shireen AbuAqla kilichotekelezwa na wanajeshi wa Israel ndani ya ardhi ya Palestina.

 

Shireen AbuAqla aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa wakati akiendelea na shughuli yake ya kuripoti habari za matukio ya unyanyasaji na mauaji yanayofanywa na majeshi ya Israel katika Kambi ya Wakimbizi ya Jenin.

 

Mwandishi wa habari huyo mkongwe wa Shirika la Utangazaji la Al-Jazeera aliuawa huku akiwa amevaa nguo maalumu yenye nembo ya kuonesha kuwa yeye ni mwandishi wa habari ambayo huvaliwa mahususi kwa ajili ya kuwakinga waandishi wa habari na hatari wakati wa machafuko au vita.

 

Ubalozi wa Palestina umeomba vyombo vya habari vyote nchini Tanzania kupaza sauti kwa pamoja na kupinga kitendo cha mauaji ya mwandishi wa habari mwenzao Shireen AbuAqla.

Shireen AbuAqla akiwa katika kambi ya wakimbizi ya Jenin

Mwandishi mwingine wa Al-Jazeera Ali Samoudi alinusurika kifo baada ya kupigwa risasi mgongoni, taarifa zinadai kuwa hakukuwa na maandamano yoyote yale kutoka kwa raia wa Palestina katika eneo la tukio hiyo inamaanisha waliwalenga waandishi wa habari ili wasiweze kukusanya habari za ukatili wanaoutekeleza katika kambi ya Jenin lakini pia wakiwa na lengo la kuwaogopesha waandishi wa habari wasiende kukusanya habari za ukatili zinazoweza kutokea baadaye.

 

 

Leave A Reply