The House of Favourite Newspapers

Ubaya Ubwela kuibukia Uwanja wa Mkapa Agosti 8


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa Ubayaubwela utaibukia Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kwenye Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.
Simba Julai 24 2024 ilifanya uzinduzi wa uzi mpya wa msimu wa 2024/25 Morogoro katika hifadhi za Mikumi ambazo zimeanza kuuzwa Tanzania nzima.
Agosti 3 2024 itakuwa ni Simba Day ambapo wachezaji wapya na waliokuwa na kikosi msimu uliopita watatambulishwa rasmi kwa mashabiki.


Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wataendelea na ubaya ubwela mpaka Agosti 8 katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii.
“Ule ubaya ubwela utaendelea na tumeona kwamba Agosti 8 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii basi tunafanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu muhimu Uwanja wa Mkapa.”

#EXCLUSIVE: ESHA BUHETI APIGA KWENYE MSHONO – “SHILOLE KAZOEA KUPIGA MABWANA ZAKE – MIMI HANIWEZI”..