The House of Favourite Newspapers

Ubingwa Wampa Kigugumizi Haaland… Afunga Mabao 50 Man City

0
Staa wa Manchester City, Erling Haaland.

STAA wa Manchester City, Erling Haaland ameshindwa kuzungumza kutokana na furaha ya kutwaa ubingwa wa Premier League ukiwa msimu wa kwanza.

Haaland ambaye ni mfungaji bora wa Premier League akiwa na mabao 36, alishindwa kufunguka wakati timu hiyo ikishangilia ubingwa wake.

Staa huyo ambaye amejiunga na Man City msimu huu akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani, tayari amevunja rekodi kibao ndani ya Premier League hasa katika upachikaji wa mabao.

Amefunga mabao 36 ndani ya ligi, huku akiwa amefunga zaidi ya mabao 50 katika michuano yote msimu huu.

“Niwe muwazi, sijui hata nini niseme. Siamini  lakini nina furaha sana kwa hiki ambacho tumefanya,” alisema Haaland.

Haaland ana nafasi nyingine ya kushinda mataji msimu huu kwani Man City inasubiri kucheza fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan na Kombe la FA dhidi ya Manchester United.

Pia Haaland anawania tuzo mbili ndani ya Premier League, mchezaji bora wa msimu na mchezaji mdogo bora wa msimu.

YANGA HAWATANII! MAYELE HAUZWI/ JEURI ya MO, SIMBA SC YAVAMIA YANGA, AZAM | KROSI DONGO

Leave A Reply