The House of Favourite Newspapers

Ubunge + Singeli = Prof Jay

0

prof jayMUZIKI wa Bongo Fleva kwa sasa ni biashara kubwa, umefika mbali kwa maana ya kutoka nje ya mipaka ya nchi na vijana wengi wa sasa wanaojiingiza kwenye muziki huo wanaona matunda yake.

Lakini pia, baadhi ya wasanii wanaofanya muziki huu hawajui chimbuko hasa ulipotokea, japo ukweli uko wazi kwa miaka ya 80 na 90 kulikuwa na makundi na wasanii mbalimbali walioufanikisha muziki huu kuchomoza.

Miongoni mwa makundi na wasanii hao wakongwe ni Fresh XE Mtui, Kwanza Unit, Diplomatz, Gangstar With Matatizo (GWM), Wagumu Weusi Asilia,Young Da’ Mob, II Proud, Saleh Jabir, Samia X, Jotwa Jokeri, Bugz Malone, Sos B, Mawingu Band, Connie Francis, Jungle Crewz Posse, Ras Pompidou, Mac Mooger, Ericka au E-Attack, Bantu Pound, Hardcore Unit na wengine kibao.

Pia kulikuwa na Kundi la Hard Blasters Crew ambalo liliundwa na wakali kama Big Willy, Terry Fanani na Joseph Leonard Haule au ukipenda waweza kumuita Prof Jay.

Mbali na kundi lake, Jay kama msanii wa kujitegemea (solo) ni miongoni mwa wakongwe waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuufikisha muziki huu hapa ulipo, ambao leo hii unaonekana kuheshimika kwa rika zote.

Ameshafanya ngoma kibao ambazo zimewahamasisha vijana wengi na kujiingiza kwenye muziki huo. Miongoni mwa ngoma zake zilizotikisa ni Chemsha Bongo, Bongo Dar es Salaam, Zali la Mentali, Nikusaidiaje, Ndiyo Mzee na nyingine kibao.

Jay kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia Chadema, lakini bado anaendeleza harakati zake za muziki. Hivi karibuni ameibuka na ujio mpya wa Kazi Kazi akiwa amemshirikisha mkali wa nyimbo za Singeli, Sholo Mwamba.

Over Ze Weekend kupitia Global TV Online limenasa mahojiano yake na katika makala haya, anafunguka zaidi;

Over Ze Weekend: Nini kilikuvutia kufanya Muziki wa Singeli?

Jay: Muziki wa Singeli ni moja kati ya muziki ambao una asili yetu kwa maana ndani ya Singeli kuna Mdundiko, Chakacha na Mdumange. Katika mawazo yangu niliona tunaweza kuleta revolution ya Hip Hop ninayoifanya. Badala ya kukopy miziki ya kina Lil Wayne na Jay Z basi tunaweza kutafuta kitu chenye Utanzania wetu tukastiki kwenye Hip Hop yetu ndiyo maana huku nimechana ila nikavalisha kitu cha utofauti yaani Singeli.

Over Ze Weekend: Bungeni wanakuchukuliaje kama mwanamuziki na pia kama mbunge?

Jay: Nilipochaguliwa kuwa mbunge, niliingia Dodoma siyo kama Profesa Jay bali ni kama Mbunge wa Mikumi. Nilikutana na mawaziri, wabunge na wengine wote. Walikuwa wakiniambia profesa usije ukaacha muziki uliokuwa ukifanya. Usije ukaacha kusapoti muziki wa Tanzania kwa sababu tumeuelewa. Sasa hivi ni kweli muziki umekwenda na kukubalika kwa rika zote, tunatakiwa kuwa na busara, hekima na kuimba vitu vinavyohusu Tanzania yetu, maana sanaa ina nguvu kuliko siasa na kama mlivyoona kwenye mataifa mengi watu wameweza kunufaika kupitia muziki. Pia hii ni nafasi pekee ya kurudi kwa mashabiki wangu, japo niko bize, nitakuwa nikiwadokolea mojamoja, paap! paap!

Over Ze Weekend: Utofauti kati ya Profesa Jay mbunge na wa kawaida upi?

Jay: Mwanamuziki ana nguvu kuliko mwanasiasa. Kabla sijaenda Dodoma kuapa kuwa mbunge nilikuwa mbunge ndani ya mitaa. Nyimbo zangu nyingi zimekuwa zikiwapa nguvu kwa wale waliokata tamaa. Kila siku nasema profesa ni voice of the voiceless. Sauti yangu na ile ya wasioweza kusikika, pia sauti yangu ni ya mtaa na ndiyo maana ngoma yangu mpya nimeita Kazi Kazi kwa wale wasiokata tamaa. Video tumeishutia Manzese (Dar) Uwanja wa Fisi kwa sababu kule kuna maisha magumu lakini nilitaka kuwaambia waliokata tamaa, Jay ni mtu aliyetokea geto lakini sasa ni mbunge, hata wewe ukikomaa unaweza. Kwenye muziki wasanii wengi wana akili sana lakini waoga wa kuthubutu wanasubiri kupewa vyeo vya kuhongwa meen!

Over Ze Weekend: Unauzungumziaje muziki wa Bongo Fleva kwa sasa?

Jay: Wasanii wawe kitu kimoja, kwa maana wana vilio kama 200 wanashindwa kuwa na umoja. Nashukuru serikali inaonekana kuweza kusaidia kwa sababu juzi tulikuwa na waziri kivuli pamoja na Waziri Nape tukiangalia jinsi tunavyoweza kuwasaidia wasanii.

Jay ameongea mengi. Kupata zaidi tembelea www.globaltvtz.com pia mahojiano yake zaidi juu ya siasa na maisha yake kwa ujumla yatapatikana hivi karibuni k

Leave A Reply