The House of Favourite Newspapers

UBUNGO YAKAMILISHA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO

0
Meya Jacob akizungumza na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Ubungo walioambatana kwenye ukaguzi wa miradi.

Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Manispaa Mpya ya Ubungo jijini Dar ikiongozwa na mwenyekiti wake, Mstahiki Meya Boniface Jacob, imemaliza ukaguzi wa miradi yake ya maendeleo kwa robo ya nne ya Mwaka wa Fedha wa 2016/2017, hata kabla ya kikao chake cha Baraza la Madiwani.

…Akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Golani.

Akizungumzia ukaguzi huo, Meya Jacob amesema kuwa, ziara za ukamilishaji wa ukaguzi huo katika kata 14, zimehitimishwa kwa kamati za kudumu za halmashauri hiyo kupata wasaa wa kujionea mabadiliko makubwa ya maendeleo.

 

“Tumejitahidi na tunaendelea kuhakikisha tunakidhi kiu ya kero za wananchi dhidi ya sekta za afya, elimu, miundombinu, masoko na miradi ya maji.

…Akiwa kwenye msafara na maafisa mbalimbali kwenye ukaguzi huo.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ukarabati wa Zahanati ya Kata ya  Mavurunza, ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Golani na ujenzi wa madarasa matatu ya Shule ya Msingi Temboni.

Meya Jacob akikagua matundu ya vioo kwenye Shule ya Msingi Msumi.

Miradi mingine ni ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Maramba-Mawili, ukamilishaji wa madarasa matatu ya Shule ya Sekondari Kiluvya, ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Msingi Msumi, ujenzi wa darasa moja la Shule ya Msingi Kawawa, ujenzi wa mfumo wa maji-taka kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina na mradi wa kisima na tanki la maji kwenye mtaa wa Gogoni,” alisema Meya Jacob.

Meya Jacob akikagua ujenzi wa Zahanati ya Mavurunza.

 

STORI NA PICHA: SIFAEL PAUL/GPL

Leave A Reply