The House of Favourite Newspapers

UBUYU: DIANA, ASLAY MAMBO NI MOTO!

KAMA unavyoujua Ubuyu ulivyo, ukiupata mbaya hakuna hata atakayeusogelea kwa sababu madhara yake unachubua ngozi ya mdomo. Lakini ukipata mzuri raha inakuja pale mnapoumung’unya wengi.

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa Isihaka Nassoro ‘ Dogo Aslay’ na muigizaji aliyetamba siku za nyuma Diana Kimari, wamezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya uhusiano wao wa kimapenzi kuibuka ghafla kama mvua.

 

Mwanamuziki Aslay, ambaye hivi karibuni alimwagana na mzazi mwenzie Tessy na kukaa kimya kiduchu bila kumuonesha mpenzi mpya; wiki moja iliyopita alionekana na msanii huyo wakiwa katika picha mbalimbali za kimahaba huku wakijibizana kwenye mitandao ya kijamii maneno yanayoashiria kuna ulimwengu wao wa kimapenzi wanaouishi hivi sasa.

MSIKIE DIANA

Gazeti hili baada ya kuona ‘mapichapicha’ hayo mtandaoni lilianza kumtafuta Diana, ambapo alipoulizwa kuhusu madai ya ‘kubanjuka’ kimapenzi na Aslay alifunguka hivi:

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Diana,napenda kujua nini kinaendelea kati yako na Aslay; maana wenye ubuyu wao wanaona kama kuna mahaba fulani hivi yamechipuka?

Diana: Mapenzi tena, Kwa nini umeniuliza hivyo?

Ijumaa Wikienda: Haha…wadau wanaona kwenye mitandao ya kijamii mnavyojiachia na picha za kimahaba; ndiyo hao wanataka kuumung’unya ubuyu.

Diana: Hata mimi sijui, ndiyo hivyohivyo wanavyoona.

Ijumaa Wikienda: Wameona mahaba! Halafu inasemekana wewe ndiyo chanzo cha ugomvi wa Aslay na mzazi mwenzie?

Diana: Yaani kwa kweli kuhusu hilo ndiyo sifahamu kabisa. Mimi ninachojua Aslay ni mtu wangu wa karibu.

Ijumaa Wikienda: Lakini wewe si uliokoka na ukawa uko mstari wa mbele kanisani imekuaje sasa na skendo hiyo na ulisema umetulia kabisa?

Diana: Jamani; kwani mtu ukiokoka maisha mengine unakatazwa kuendelea nayo?

Ijumaa Wikienda: Sasa wachungaji wako wanapoona picha zako za kimahaba mtandaoni wanakuelewaje?

Diana: Jamani kanisani wanaenda wenye dhambi na wasiokuwa nazo, lakini wachungaji wanawapenda zaidi wenye dhambi ili wawarudishe kundini na kingine kama wakijua ukweli wa jambo linalosemwa kuwa si la kweli wala hawaangaiki.

Ijumaa Wikienda: Ila kuna tetesi mnaishi pamoja na Aslay?

Diana: Sitaki kuzungumzia hilo mimi.

Gazeti hili liliamua kumuweka kando Diana na kufanya jitihada za kumtafuta Tessy, ambapo alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema kuwa hawezi kuzungumzia ishu hiyo watafutwe wahusika

“Nafikiri wangetafutwa wenyewe ingekuwa ni vizuri zaidi maana wao ndiyo wahusika” alisema Tessy.

Baada ya kuzungumza na warembo hao Wikienda lilimvutia simu Aslay ambapo alipobanwa kuhusu hilo alifunguka kama ifuatavyo.

Ijumaa Wikienda: Vipi kaka ndiyo umeamua kummwaga Tessy moja kwa moja na kujiweka kwa Diana.

Aslay: Unajua dada yangu,nipo tayari kukuelezea lakini sasa naingia studio kwanza.

Ijumaa Wikienda: Lakini si unijibu tu kidogo.

Aslay: Nafikiri niseme kiufupi tu mwenye macho aambiwi tazama.

Na Imelda Mtema : Ubuyu Uliyonyooka

Comments are closed.